Chloe atahamia Zanzibar kwasababu mama yake ataanza kufanya kazi kisiwani hapo kama
mwanabiolijia wa sayansi za bahari. Mara tu atakapowasili Chloe ataanza kutembelea ulimwengu
wa chini ya maji pamoja na mwanafunzi mwenzake mpya Amo. Walipokua wanaogelea baharini
walikutana na nguva aliyeitwa Nya. Akawaonyesha nyumbani kwake - uwanda wa majani bahari
unaoundwa na majani mabichi manene hadi macho yanapoweza kuona. Katikati ya maji wanaona
Wanyama wa kila aina ya rangi. Chloe na Amo wanavutiwa mara moja na maajabu haya ya chini ya
maji. Hata hivyo wanaporudi wiki chache baadaye kwenye ufuo huo baada ya majira ya joto kali
nyasi za baharini zimetoweka pamoja na rafiki yao Nya. Lilibakia jangwa la mchanga tu. Ni nini
kilitokea na wanaweza kufanya nini? Chloe na Amo wakajipanga kurudisha msitu wao wa chini ya
maji.